Mkurugenzi wa Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini IRDO(Integrated Rural Development Organization) Dr. Simon Chiwanga amepokea ugeni wa SSP. K.J.Msukwa ambae ni mkuu wa jeshi la Polisi wilaya ya Momba (OCD), A/INSP M.C.Myumvi ambae ni Afisa Mkaguzi Kata ya Majengo, Sajenti. Irene Mtende kutoka kitengo cha kuzuia dawa za kulevya ngazi ya polisi, ugeni huo ulipokelewa katika nyumba ya kupunguza madhara ya dawa za kulevya (DIC) na baadae katika ofisi ya Shirika iliyopo Chapwa. Lengo la ugeni huu ni kutembelea na kufahamu miradi inayofanywa na Shirika la Uwiano wa Maendeleo vijijini. Aidha Ugeni huo uliambatana na wafanyakazi kutoka kituo cha Dawa mbadala kwa ajili wa waraibu wa dawa za kulevya (MAT) ambao ni Dr. Peter Mapunda ambae ni meneja wa MAT na Happy Matao. Wageni walifanikiwa kutembelea mradi wa DREAMS, mradi wa udhibiti wa UKIMWI na Kinga na mradi wa MAT ambapo wageni walipata fursa ya kuona namna shirika linasaidia vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia fani mbali mbali kama ushonaji na uoteshaji wa miche ya maua na matunda. Pamoja na hayo Mkurugenzi wa Shirika alieleza nia yake ya kuanzisha klabu mbalimbali mashuleni ambazo zitakua zinapinga masuala ya Ukatili wa kijinsia, matumizi ya dawa za kulevya na masuala ya Virusi vya UKIMWI.