Mkurugenzi wa Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini/IRDO Dr. Simon Chiwanga ametembelewa na Idara ya Masomo ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Mzumbe na kutembelea ofisi za shirika pamoja na miradi inayotekelezwa na shirika ambayo ni HIV Prevention Care and Support, DREAMS na FOSENI II (Food Security and Nutrition Improvement) kwa lengo la kuona ni maeneno gani ambayo yanaweza kuboresha zaidi ushirika wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini. Katika ziara hiyo timu ya Chuo Kikuu cha Mzumbe ilieleza kua imejifunza mengi sana kwenye miradi inayotekelezwa na shirika na wameona maeneo mengi ambayo yanaweza kuboresha zaidi uhusiano ulipo kati ya shirika na Chuo Kikuu cha Mzumbe kama vile:- Kushauri na kusaidia kwa namna gani bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika wa mradi wa DREAMS zifike sokoni vile vile kutoa msaada wa hakimiliki ya umiliki wa bidhaa hizo wanazotengeneza, kushilikiana kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari juu ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya na Mimba za utotoni vile vile kusaidia waraibu wa dawa za kulevya ambao tayari walishaanza matibabu ya Methadone mahitaji muhimu kama vile mavazi, kutoa mafunzo mafupi kwa lengo la kujengea uwezo shirika na wafanyakazi wake, pia kutoa ushauri kutoka kwa wataalamu wa mazingira, ukusanyaji data na mambo mengine mengi ambayo wanaweza kushirikiana na shirika