info@irdo.or.tz +255 719 547 460

Ziara ya Mkurugenzi wa shirika la Uwiano Wa Maendeleeo Vijijini/IRDO pamoja na Maafisa waandamizi wa shirika iliyofanyika kuanzia tarehe 12 february hadi tarehe 23 february 202

Kikundi cha Ushindi kilichopo kijiji cha Ishinga,Kata ya Itale, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe

Posted on: February 12, 2024
Mkurugenzi wa shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini IRDO/Integrated Rural Development Organization Dr. Simon Chiwanga amefanya ziara kutembelea mradi wa FOSEN/Food Security and Nutrition Improvement (Uhakika wa Chakula na Uboreshaji wa Lishe) pamoja na uongozi wake wa juu Wakiongozwa na Mratibu wa mradi Mr. Gaster Kihwello Wamefanikiwa kukutana na wanufaika wa mradi katika kikundi cha Ushindi kilichopo kijiji cha Ishinga,Kata ya Itale, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe kwa lengo la kujua wamenufaika vipi na mradi na kutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ileje pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe

Posted on: February 13, 2024
Katika Ziara ya Mkurugenzi wa shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini Dr.Simon Chiwanga Akiambana na Maafisa Waandamizi wa shirika Walitembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ileje pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe Kuendeleza Uhusiano wao katika utekelezaji wa Miradi ikiwemo mradi wa FOSENI/Food Security and Nutrition Improvement (Uhakika wa Chakula na Uboreshaji wa Lishe) unaotekelezwa kwa sasa Wilaya ya Ileje.

Kikundi cha Tusongembele Kilichopo kijiji cha Ibungu,kata ya Bupigu, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe

Posted on: February 13, 2024
Mkurugenzi wa Shirika la Uwiano Wa Maendeleo Vijijini IRDO/Integrated Rural Development Organization Dr.Simon Chiwanga, Maafisa waandamizi wa Shirika wakiongozwa na Mratibu wa Mradi wa FOSEN/Food Security and Nutrition Improvement (Uhakika wa Chakula na Uboreshaji wa Lishe) Mr. Gaster Kihwello ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Walifanikiwa kutembelea wanufaika wa mradi wa FOSENI kikundi cha Tusongembele Kilichopo kijiji cha Ibungu,kata ya Bupigu, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe pamoja na moja ya shughuli wanazo fanya kama kikundi ambayo ni Ufugaji kuku.

Kituo cha kulelea watoto yatima cha Isoko(Isoko Orphan Project)kilichopo kijiji cha Isoko, kata ya Kafule, Wilaya ya Ileje , Mkoa wa Songwe

Posted on: February 13, 2024
IRDO_Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika Dr.Simon Chiwanga imefanikiwa kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Isoko(Isoko Orphan Project)kilichopo kijiji cha Isoko, kata ya Kafule, Wilaya ya Ileje , Mkoa wa Songwe na kutoa baadhi ya mahitaji ikiwepo pikipiki kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Ndugu, Enea Kajange ambayo itawasaidia katika majukumu yao ya kila siku katika kituo hicho.

Kaya mojamoja ya Wanufaika wa Mradi wa FOSENI kijiji cha Malangali,Kata ya Malangali, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe

Posted on: February 14, 2024
Mratibu wa Mradi wa FOSENI/Food Security and Nutrition Improvement (Uhakika wa Chakula na Uboreshaji wa Lishe) Gaster Kihwello akiongozana na Maafisa Waandamizi wa Shirika la @irdo_tanzania Walitembelea kaya mojamoja ya Wanufaika wa Mradi wa FOSENI kijiji cha Malangali,Kata ya Malangali, Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe kuona Mafanikio waliyopata kutoka kwenye mradi ikiwa ni Ufugaji wa Kuku na Utengenezaji wa Mbolea/Mboji Asili(Mashimo Matatu) na Mashamba/Bustani ambazo wametumia mbolea/Mboji hizo asili.

Wanufaika wa mradi wa DREAMS; AGYWs/Adolescent Girls And Young Women (Wasichana Rika Balehe na Wanawake Vijana miaka 15 hadi 24) wanaopata mafunzo ya cherehani katika kituo kilichopo Ofisi za IRDO, Kata ya Chapwa, Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkoa wa Songwe

Posted on: February 15, 2024
Maafisa waandamizi wa shirika la Integrated Rural Development Organization (IRDO) wakiongozwa na Mratibu wa Mradi Bi. Eva Rweyemamu waliotembelea wanufaika wa mradi wa DREAMS; AGYWs/Adolescent Girls And Young Women (Wasichana Rika Balehe na Wanawake Vijana miaka 15 hadi 24) wanaopata mafunzo ya cherehani katika kituo kilichopo Ofisi za IRDO, Kata ya Chapwa, Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkoa wa Songwe kwa lengo la kujua maendeleo ya mradi na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwa wanufaika hao.

Eneo linalotumika kwa mapumziko na kupata elimu Kwa waraibu wa dawa za kulevya DIC (Drop-In Center)

Posted on: February 16, 2024
Maafisa waandamizi wa shirika la IRDO/Integrated Rural Development Organization wakiongozwa na Mratibu wa mradi wa Kuzuia na Kupambana na VVU (HIV Prevention Care and Support) Bwana. Amon Mlawa walitembelea eneo linalotumika kwa mapumziko na kupata elimu Kwa waraibu wa dawa za kulevya DIC (Drop-In Center) kujua maendeleo na kutatua changamoto za waraibu wa madawa ya kulevya wanao pata huduma ndani ya DIC(Drop-In Center) na kujua maendeleo ya shughuli zao za kujiongezea kipato IGA (Income Generating Activities).

eneo salama (Safe Space) linalotumika na mabinti wanufaika wa mradi AGYWs/Adolescent Girls and Young Woman (Wasichana Rika Balehe na Wanawake Vijana umri miaka 15 hadi 24) katika kikundi cha Strong Girls kilichopo kata ya Katete, halmashauri ya mji Tunduma , mkoa wa Songwe

Posted on: February 16nd, 2024
Maafisa waandamizi wa shirika la IRDO/Integrated Rural Development Organization wakiongozwa na Mratibu wa mradi wa DREAMS Bi. Eva Rweyemamu walitembelea eneo salama (Safe Space) linalotumika na mabinti wanufaika wa mradi AGYWs/Adolescent Girls and Young Woman (Wasichana Rika Balehe na Wanawake Vijana umri miaka 15 hadi 24) katika kikundi cha Strong Girls kilichopo kata ya Katete, halmashauri ya mji Tunduma , mkoa wa Songwe kujua maendeleo, kusikiliza na kutatua changamoto kutoka kwa wanufaika hao wa mradi AGYWs moja ya changamoto waliyo tatua ni kuchangia shilingi 150,000/= Katika kikundi cha Strong Girls kama Hamasa kwa Wanakikundi

Wanufaika wa mradi wa DREAMS; AGYWs/Adolescent Girls And Young Women (Wasichana Rika Balehe na Wanawake Vijana miaka 15 hadi 24) kikundi cha Peace Dadas kilichopo mtaa wa Ipito, kata ya Mpande, Halmashauri ya mji Tunduma, mkoa wa Songwe

Posted on: February 22nd, 2024
Maafisa waandamizi wa shirika la Integrated Rural Development Organization (IRDO) wakiongozwa na Mratibu wa Mradi Bi. Eva Rweyemamu waliotembelea wanufaika wa mradi wa DREAMS; AGYWs/Adolescent Girls And Young Women (Wasichana Rika Balehe na Wanawake Vijana miaka 15 hadi 24) kikundi cha Peace Dadas kilichopo mtaa wa Ipito, kata ya Mpande, Halmashauri ya mji Tunduma, mkoa wa Songwe, Kwa lengo la kujua maendeleo yao na kutatua changamoto mbalimbali, moja ya mafanikio ya kikundi hicho ni kutumia ujuzi waliopata kwenye mafunzo chini ya DREAMS ya kutengeneza sabuni za maji zinazowaingizia kipato. Viongozi wa IRDO wamepata fursa ya kununua bidhaa hizo zenye ufanisi mkubwa kwenye matumizi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh. Dkt.Francis K. Michael

Posted on: February 22, 2024
Mkurugenzi wa shirika la IRDO/Integrated Rural Development Organization Dr. Simon Chiwanga pamoja na maafisa waandamizi wa shirika wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh. Dkt.Francis K. Michael kwa lengo la kumkaribisha katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Shirika (Strategic and Resource Mobilization Plan) wa miaka mitano ijayo (2024-2028) utakayofanyika tarehe 5/3/2024, Staples Hall, Tunduma - Songwe. Pia walifanikiwa kutoa Tathmini ya Maendeleo ya baadhi ya miradi inayotekelezwa na shirika kwa mkoa wa Songwe ikiwemo FOSENI(Food Security and Nutrition Improvement) - Ileje; DREAMS - Tunduma na HIV Prevention, Care and Support -Tunduma na Momba na ni kwa jinsi gani miradi hiyo imeleta matokeo chanya kwenye Uhakika wa Chakula, Uboreshaji Lishe, Afya ya Jamii/Mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI, Mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia na Elimu na Ujuzi katika Mpango wa kuinua uchumi wa vijana na mabinti wa rika balehe, wanawake na wanaume vijana katika jamii ya Mkoa wa Songwe. Mkuu wa Mkoa ameushukuru uongozi wa shirika kwa kusimamia miradi vizuri na ameahidi kutoa ushirikiano yeye na uongozi wa Mkoa na Wilaya husika kwenye miradi hiyo

Vikundi vya Vijana vya Upendo Group na Umoja Group na kikundi cha Tupendane cha Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, vyote vilivyopo kata ya Kamsamba, wilaya ya Momba, mkoa wa Songwe

Posted on: February 22, 2024
Mkurugenzi wa shirika la Uwiano Wa Maendeleo Vijijini IRDO/Integrated Rural Development Organization Dr. Simon Chiwanga pamoja na maafisa waandamizi wa shirika wameendelea na ziara ya kutembelea miradi ya shirika na walifanikiwa kutembelea vikundi vya Vijana vya Upendo Group na Umoja Group na kikundi cha Tupendane cha Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, vyote vilivyopo kata ya Kamsamba, wilaya ya Momba, mkoa wa Songwe. Kwa upande wa vikundi vya vijana wanufaika wako chini ya kitengo cha Enabling DREAMS inayohusisha AGYWs (Wasichana Balehe na Wanawake Vijana) na ABYWs (Wavulana Balehe na Wanaume Vijana). Wawezeshaji walitoa elimu ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI, VMMC (Tohara ya Wanaume Kwa Hiari, PrEP(Pre Expouser prophylaxis), namna ya kujikinga na magonjwa ya zinaa na Eelimu juu ya uzazi wa mpango.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba,mkoa wa Songwe

Posted on: February 23, 2024
Mkurugenzi wa shirika la IRDO/Integrated Rural Development Organization Dr. Simon Chiwanga pamoja na maafisa waandamizi wa shirika wameitembelea ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba kutambulisha mradi wa Enabling DREAMS unaohusisha AGYWs (Wasichana Balehe na Wanawake Vijana), ABYWs (Wavulana Balehe na Wanaume Vijana) kuendelea kujenga uhusiano wa kiutendaji kati ya serikali na shirika. Enabling DREAMS ni afua inayotekelezwa chini ya Mradi wa Kudhibiti UKIMWI (HIV Prevention, Care and Support) wilayani Momba. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri amesisitiza shirika kupitia mradi huu liwasaidie vijana kuwajengea uwezo wa kiufundi na biashara kupitia vikundi ili kuondokana na tabia zilizokithiri za kukaa vijiweni na kujihusisha na vitendo viovu mitaani.

Waelimishaji rika (Peer Educators), Amon na Agnes kutoka Kata ya Ndalambo wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe

Posted on: February 23, 2024
Waelimishaji rika (Peer Educators), Amon na Agnes kutoka Kata ya Ndalambo wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe wakielezea utendaji kazi, mafanikio na changamoto za mradi wa Enabling DREAMS na VMMC (Tohara ya Wanaume kwa Hiari). Ni afua inayotekelezwa chini ya Mradi wa Kudhibiti UKIMWI (HIV Prevention, Care and Support). Hayo yamefanyika katika kituo cha afya cha Ndalambo chini ya Mganga Mfawidhi Dr. Ng'halanga Malimi na ujumbe wa IRDO chini ya Mkurugenzi Dr. Simon Chiwanga pamoja na maafisa waandamizi wa shirika.